DStv Inogilee!

Shuhudia Ufaransa dhidi ya Ujerumani, England Vs Hispania michuano ya UEFA Nations League ndani ya DStv wiki hili

Kampuni ya DStv inakuletea mashindano mapya ya UEFA Nations League yanayo tarajia kuanza kutimua vumbi wiki hii kwa kuikutanisha miamba ya soka ambao ni mabingwa wa kombe la dunia mwaka huu timu ya taifa ya Ufaransa dhidi ya Ujerumani siku ya Alhamisi.

Kunako Ijumaa taifa dogo duniani, Albania itashuka dimbani kuwakabili Israel huku Italia ikiwa mwenyeji dhidi ya Poland wakati mchezo wa mwisho ukiwa ni baina ya Uturuki watakao wavaa wenyeji wa michuano ya kombe a dunia mwaka huu timu ya taifa ya Urusi.

Kwenye michuano hiyo inayotarajiwa kuwa na mvuto mkubwa kutokana na ukubwa timu zinazo shiriki siku ya Jumamosi Uswis itakuwa na kibarua dhidi ya Iceland wakati Finland ikicheza na Hungary huku taifa pendwa katia soka England wakiwa na kibarua kigumu mbele ya Hispania.

Miamba ya soka ya Ujerumani wakishuka Jumapili kuwakabili Peru wakati Ufaransa ikicheza na Netherlands huku Bulgaria wakiiva Norway na Denmark wakicheza mbele ya Wales.

Kupitia DStv ndani ya Supersport 8 kifurushi Bomba kwa sh.19, 000 pekee Jumamosi hii ya Septemba 8, inakupatia mubashara mtanange wa kukata na shoka baina ya wenyeji Uganda ‘The Cranes’ dhidi ya timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ zote kutoka Afrika Mashariki mchezo wa kutafuta tiketi ya kufuzu michuano ya Afcon.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW