Aisee DSTV!
SwahiliFix

Shuhudia Waziri Mwakyembe akirukaruka kwa furaha baada ya Taifa Stars kuifunga Burundi na kusonga mbele (+video)

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe na Rais wa TFF Wallace Karia hapo jana wameonekana wakifurahia ushindi wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars dhidi ya Burundi.

Viongozi hao wameonekana wakirukaruka na kupiga mayowe wakiwa pamoja na wachezaji katika vyumba vya kubadilishia nguo.

Tanzania inatinga hatua ya makundi katika kusaka tiketi ya kufuzu Kombe la Dunia mwaka 2022 nchini Qatar kwa ushindi wa penati 3-0 kufuatia sare ya bao 1-1 kwenye mchezo wa marudiano uliyopigwa hapo jana siku ya Jumapili. Tanzania 1-1 Burundi (Agg: 2-2)

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW