Aisee DSTV!
SwahiliFix

Shujaa Juma Kaseja afunguka kuhusu uwezo wake ”Kwenye maisha yangu sijawahi kufundishwa kudaka Penati”(+video)

Timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars hapo jana ilifanikiwa kusonga mbele kwenye hatua ya makundi michuano ya kombe la dunia baada ya kuifunga Burundi katika mwikwaju ya penati.

Taifa Stars ikiishinda kwa penati 3-0 kufuatia sare ya bao 1-1 kwenye mchezo wa marudiano uliyopigwa hapo jana siku ya Jumapili. Wakati kwenye milingoti mitatu kukiwa na shujaa aliyeibeba Tanzania, Juma Kaseja ambaye alizicheza penati za Burundi na kuambulia patupu.

Waswahili husema Ng’ombe hazeeki maini, baada ya kuibuka nyota wa mchezo mkongwe Juma Kaseja akasema ufundi wake wa kuzidaka penati hajafundishwa na mtu na kwa sasa unaenda mwaka 19 akiwa bado yupo fiti ligi kuu soka Tanzania Bara.

”Unaenda mwaka wa 19 nacheza Ligi Kuu, lakini kwenye maisha yangu hakujawahi kuwa na Mwalimu wa kuja kunifundisha kudaka penati, nadhani ni kipaji tu kanipa Mungu na Mungu huwa anambariki yeyote anayemtaka, naamini nimebarikiwa,“

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW