Habari

Shule ina wasiojua kusoma asilimia 70

ASILIMIA 72 ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Nyamatoke iliyoko Kata ya Nyamatare Tarafa ya Ikorongo wilayani hapa Mkoa wa Mara, hawajui kusoma na kuandika.

Na Anthony Mayunga, Serengeti


ASILIMIA 72 ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Nyamatoke iliyoko Kata ya Nyamatare Tarafa ya Ikorongo wilayani hapa Mkoa wa Mara, hawajui kusoma na kuandika.


Uchunguzi uliofanywa na Mwananchi na kuthibitishwa na Ofisi ya Mkaguzi wa Shule ya Msingi Wilaya ya Serengeti, umebaini kuwepo kwa tatizo hilo.


Shule hiyo ambayo ni miongoni mwa shule saba zilizofanya vibaya kiwilaya na kimkoa katika mtihani wa taifa wa darasa la saba wa mwaka jana ina walimu watano kwa kipindi kirefu na kubakia wanne baada ya ofisi ya elimu wilaya kumhamisha mmoja .


Walimu, viongozi wa kijiji na baadhi ya wazazi waliliambia Mwananchi kuwa, shule hiyo yenye wanafunzi 458 inakabiliwa na uhaba wa walimu, vitabu, madawati, matundu ya vyoo na nyumba za walimu.


‘ Unavyoona ofisi yetu haina hata meza wala viti ,sasa katika hali kama hii unategemea nini katika maendeleo ya shule miujiza gani itatokea hapa/ � Alihoji mmoja wa walimu.


Uchunguzi zaidi ulibaini pkuwa utoro wa wanafunzi pia umesababisha asilimia 44 ya wanafunzi kufanya vibaya katika matokeo ya mtihani wa darasa la saba mwaka jana na kwamba wanafunzi 20 kati ya 56 hawakufanya.


Mwananchi pia limebaini kuwapo kwa uhusiano mbaya kati ya walimu wa shule hiyo na wanakijiji kitu na kusabisha wanakijiji hao kukata mazao ya walimu na kuvunja dirisha la nyumba ya mwalimu kwa kutumia jiwe kwa lengo la kuwatisha.


Kwa upande wa wanafunzi waliohojiwa na gazeti hili walisema wamekuwa hawasomi kwa kipindi kirefu.


Source: Mwananchi

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents