Habari

Shule kufungwa kwa kukosa walimu

SHULE wa Msingi Makayo, iliyopo Kata ya Mkalamo, wilayani Korogwe, Tanga ipo hatarini kufungwa kutokana na kukosa walimu. Kutoka na hali hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mohame Abdulaziz, amempa siku 30 Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe Vijijini (DED), Elias Sangi, kuhakikisha anawapeleka walimu wa kutosha katika shule hiyo.

na Fina Allan, Korogwe

Mkuu huyo wa Mkoa (RC) alitoa agizo hilo baada ya kuzindua josho la kuogeshea mifugo katika Kijiji cha Makayo kinachoongoza kwa idadi kubwa ya jamii ya wafugaji. Shule hiyo ilijengwa kwa msaada wa Shirika la World Vision Tanzania na wananchi.

“Hali hii haijanifurahisha kabisa…DED nakupa siku 30 kuanzia leo (jana) walimu wawe wamefika katika Shule ya Msingi Makayo? Hii ni aibu kwa kuwa haina hata mwalimu mmoja na wanafunzi wamehamishiwa Shule ya jirani ya Pasilasi,” alisema mkuu huyo wa mkoa.

Awali, Diwani wa Kata ya Mkalamo, Luka Logani, alimweleza mkuu huyo wa mkoa (RC) kuwa wanafunzi wanaosoma shule hiyo hulazimika kutembea umbali wa zaidi ya kilomita nane kwa siku hadi kufika Pasilasi, shule ya jirani walipoombewa kwa muda.

Alisema ni vigumu kwa wanafunzi hao wa jamii ya wafugaji kusoma na kumaliza darasa la saba kutokana na ukosefu wa daraja linalounganisha kijiji hicho na vijiji vya jirani ambavyo hupata msaada.

Logani alitahadharisha kuwa hata ubovu wa barabara katika vijiji vya kata hiyo kimekuwa kikwazo kikubwa wakati wa msimu wa mvua za masika, hali ambayo inachangia kukwamisha utekelezaji wa shughuli za maendeleo.

Source: Tanzania Daima

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents