Habari

Si Koffi, Acudo, Twanga, Mdebwedo… FM Academia wafunika Fiesta 2007

FM AcademiaKatika akili ya mashabiki wengi ambao walihudhuria katika viwanja vya leaders club maeneo ya kinondoni waliamini kuwa mtu mzima Koffi atafanya maajabu katika upande wa show za bolingo lakini shughuli yake ilionekana si kitu mbele ya wazee wa Ngwasuma FM Academia

FM Academia

 

Katika akili ya mashabiki wengi ambao walihudhuria katika viwanja vya leaders club maeneo ya kinondoni waliamini kuwa mtu mzima Koffi atafanya maajabu katika upande wa show za bolingo ukizingatia yeye ni mmoja katika ya waasisi wa muziki wa bolingo barani Africa lakini shughuli yake ilionekana si kitu mbele ya wazee wa Ngwasuma FM Academia.

 

FM academia ambao walionekana kupania sana siku hiyo walipanda hukwaani wakiwa wamepiga suti zao za kaki ambazo ziliwafanya waonekana smati na wenye kuvutia, wakati mtu mzima Pablo Masai alionekana akiliongoza jahazi kikamilifu mara pale walipopanda jukwaani na sebene la kufa mtu.

 

“hii ni Fiesta 2007 hatukuwa tumejipanga na ndio maana tulipopanda juu ya jukwaa tukaamua kupiga masebene tu yaliyoambatana na raping kali zenye kuwakongo mashabiki wetu pia tuna shughuli za kufanya hatukuwa na muda wa kuangalia wenzetu watafanya nini tunashukuru sana tumemaliza show na sasa tunatimua” alisema kiongozi wa bendi hiyo mara aliponaswa na mwandishi wa Bongo 5 alipokuwa akishuka jukwaani.

 

Kwa mujibu na tathmini ya jinsi onesho lilivyokuwa hakuna msanii wala kundi la muziki ambalo liliweza kufikia leo za FM academia kwa yowe, show na kulitawala jukwaa, “sawa hatukatai kuwa mkongwe kafanya show nzuri sema ameshindwa kutupa mzuka kama ambavyo tulikuwa tumetarajia si umeona mwenyewe wazaire wa kibongo walivyokamua.

 

Ilikuwa ni shangwe za hatari kwani wakati vijana hao wako jukwaani wakiendelea kuwasha moto, mvua ambayo haikujulikana ilikotokea ilianza kunyesha lakini haikusababisha wazee wa Ngwasuma kushuka jukwaani na show kusimama isipokuwa mashabiki walibeba viti vyao na kujitwisha vichwani na kuendelea na shangwe wakati mashabiki wengine waliendelea kujiachia utadhani hapakuwa na mvua.

 

Kwa ujumla Fiesta 2007 shangwe boda to boda ilikuwa ni ya FM Academia

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents