Habari

Siasa ni shule isiyokuwa na mwisho – Ridhiwan Kikwete

Katika mechi mbalimbali zinazotokea uwanja wa Taifa watu mchanganyiko huhudhuria, kuanzia mastaa wa filamu viongozi wa siasa na wananchi na kila mmoja akiwa na ushabiki wa timu yake anayoipenda.

Jumapili hii Mbunge wa Chalinze mkoani Pwani, Ridhiwan Kikwete(CCM), amesema siasa ni shule ambayo haina mwisho na ndiyo maana anaendelea kujifunza mengi kutoka kwa wanasiasa wenzake hususan waliomtangulia.

Ridhiwani ametumia Instagram kuelezea hilo baada ya kukutana na aliyekuwa mgombea urais kupitia Chadema katika uchaguzi wa mwaka 2015, Edward Lowassa katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam, wakati wa mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara kati ya Simba na Yanga.

“Siasa ni shule ambayo haina mwisho. nahisi bado niko shule ya msingi na ninaendelea kujifunza,” ameandika.

Mbunge huyo alimfuata Lowassa alipokuwa amekaa na kufanya naye mazungumzo ambayo hajayaweka wazi, na kisha kurudi sehemu yake huku akishuhudia timu yake ya Yanga iliyofungwa 2 – 1 na Simba.

Wengi wamefurahishwa na maneno hayo huku wakimpongeza mbunge huyo.

By: Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents