Burudani

Sifanyi muziki kwa ajili ya menejimenti – Barakah The Prince

Baada ya kujiondoa katika label ya RockStar4000 msanii wa Bongo Flava, Barakah The Prince amedai hafanyi muziki kwa ajili ya menejimenti bali mashabiki wake.

Muimbaji huyo amesema bado anaamini ana nyimbo nzuri lakini zinaposhindwa kufanya vizuri menejimenti inakuwa hajatekeleza wajibu wake ipasavyo na utaratibu wa kutoa ngoma mmoja kwa mwaka sio sawa kwa upande wa mashabiki wake.

“Na mwisho wa siku kazi nzuri ninazo sasa nini kinafanya kazi zifeli?, ina maana kuna vitu havikai sawa kwa upande wa usimamizi, hawafuatilii kuanzia promotion na kila kitu, bora nifanye mwenyewe sio unakuwa chini ya mtu wimbo unatoka mmoja kwa mwaka vitu vinakuwa haviendi na mwisho wa siku hii ni biashara mashabiki wangu wanakuwa wananilalamikia,” ameiambia E-Newz ya EATV na kuongeza.

“Mimi sifanyi muziki kwa ajili ya menejimenti, nafanya kwa ajili mashabiki, ndio wanadownload nyimbo zangu naingiza mtonyo, hao ndio wanaviewer nyimbo zangu YouTube nalipwa, kwa hiyo wanapolalamika Barakah hautoi wimbo halafu hakuna taarifa yoyote inakuwa inanigharimu,” amesisitiza.

Katika hatua nyingine ameongeza kuwa huwa anaangalia mafanikio ya utendaji wake wa kazi kwa kupima zile zilizopita na zinazokuja, iwapo namba zitapungua au kuongezeka anajua kazi imeenda sawa.

By Peter Akaro

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents