Burudani

Sifanyi muziki wa kushindana – Ali Kiba (+Video)

Msanii wa Bongo Fleva, Ali kiba amewachana wale wote wasanii ambao wanataka kushindana nae kwa kusema kuwa yeye katika muziki wake hakuna mtu wa kushindana  naye kwani hafanyi muziki wa kushindana na kama watafanya hivyo basi atawaacha washindane .

Ali Kiba akiwa kwenye mahojiano na Kituo cha Radio cha Capital FM

Akifunguka kwenye mahojiano yake na kituo cha Capital FM cha nchini Kenya, Ali Kiba amesema katika maisha yake ya muziki hataki kuona mtu yoyote anamtoa katika njia yake, ndiyo maana watu ambao wanakuwa wakiongea ongea sana juu yake yeye na muziki wake hawapi nafasi, kwani anaamini akiwapa nafasi wanaweza kumtoa kwenye mambo ambayo yeye amekusudia kuyafanya hasa zaidi katika muziki wake ndiyo maana hafanyi muziki kwa kushindana.

“Kila binadamu yupo na tabia yake  kuna wengine wanafanya vitu wanajua wanakosea wanafanya makusudi na kuna wengine wanaongea lakini hawajui kama wanakosea so mimi kama mwanamuziki sitaki kuwasikiliza hao  kwa sababu nina Target yangu ninavitu vya kufuatilia  sitaki  hata mtu yeyote aniingilie kwenye Target yangu kwahiyo kama utawafuatilia utapotea sifanyi muziki kwa kushindana kama hao watafanya muziki kwa kushindana nitawaacha washindane  “ alisema Ali Kiba kwenye mahojiano yake na Capital Radio ya Kenya .

Ali Kiba ambaye yupo nchini Kenya kurekodi kipindi cha Coke Studio Africa Season 5 ameahidi kuachia ngoma muda si mrefu hivyo amewataka mashabiki wasimpe presha ya kumfosi kutoa ngoma kwani muziki anaoufanya ni kwa ajili yao na kwake pia.

By Godfrey Mgallah

 

 

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents