Burudani

Sijamponda Diamond, waandishi wananiwekea maneno mdomoni – Alikiba

Alikiba ameelezea kusikitishwa kwake na taarifa iliyosambaa kuwa alitoa kauli dhidi ya Diamond kuwa anajisikia kichefuchefu kila akimsikia msanii huyo.

alikiba1

Akizungumza na Bongo5 jana, Alikiba alisema hata watu wake wa karibu wanajua hawezi kufanya jambo kama hilo.

“Hiyo mimi nimeisoma juzi na mwenyewe sijaifurahia. Vilevile na kibaya zaidi inaonesha eti kwamba mimi nimesema nikimsikia Diamond najisikia kichefuchefu, mimi namchukia Diamond,” amesema.

“Yaani kwa uelewa wangu na akili yangu timamu hata watu wanaonielewa mimi hata uwezo wa kusema hivyo sina na siwezi, kibinadamu haipendezi. Halafu huyu mwandishi aliyeandika hivi anamaanisha kabisa anapenda huu uchochezi ulipo na mabifubifu na mateam team yanayoendelea ilimradi nionekane mimi na sura mbaya katika jamii. Kwa sababu hicho kitu ni cha kutukosanisha. Huwezi kuniandika mimi nimesema live halafu kulikuwa na waandishi wengine wakati nahojiwa mbona hao waandishi wengine hawakuandika hivyo?” amehoji Kiba.

“Ushahidi wa sauti upo bana, sio kwamba unakwenda unaandika habari tofauti ilimradi nionekane mimi ni mbaya mbele ya watu. Mimi hicho kitendo kimeniudhi na sijakipenda, sijakifurahia na hii inakuwa inashusha hadhi ya kampuni kwa sababu siku nyingine watu wanavyotaka habari tutaonyesha ushirikiano mdogo kwa sababu ya vitu kama hivyo.

Watu wanaalikwa vizuri kufanya kazi ili kuwafikishia wananchi habari lakini habari zinazokwenda ni tofauti. Hii haipendezi na sijafurahishwa nayo na nimesikia watu wanatukana sana wanaongea comment tofauti tofauti.”

Katika hatua nyingine Alikiba alizungumzia kwa mara nyingine tena kuhusiana na uadui katika mashabiki wake na wale wa Diamond kwenye mitandao ya kijamii.

“Ukitaka kuzungumzia upande wa timu na unapande wa support, sisi hatusaidiani kwa kweli in general, hatusaidiani kabisaa. Na ukizungumzia upande wa team, mimi simaanishi na support hizi timu ziwepo na sina nguvu yoyote ya kumzuia mtu kufanya anachojisikia, wameshindwa watu wengi. Kulikuwa kuna ubishano wa mashabiki wa Simba na Yanga, ikija timu pinzani wanashabikia timu pinzani hivi hivi tulikuwa tunajionea hapa. Sina nguvu hiyo kwamba nitamkataza mtu kwa sababu simjui hata mmoja na nani na nani ambaye anashabikia. Mimi chakuchangia ninaweza sema tu-support vya kwetu hicho ndo kitu naweza kusema.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents