Burudani

Sijaona umuhimu wa kufanya kazi bure – Abby Dady

Producer wa hit song kama Aje na Chekecha za Alikiba, Abby Dady amedai kwa sasa ‘hasikiki’ sana kwa kuwa ameanza kuwa serious kibiashara hivyo wale wasanii waliokuwa wanarekodi bure wamekimbia.

Abby Dady amesema kwa sasa amejielekeza katika biashara zake, na zile vurugu watu walizokuwa wanazisikia ni kwa sabubu kazi nyingi zilikuwa za bure.

“Wasanii wengi utapokuwa serious basi kila msanii anakimbia, anaondoka. Kikubwa ni hicho kwamba kukaa kwangu kimya au kupunguza vurugu zilizokuwepo mwanzo kazi nyingi zilikuwa bure. Hata hawa maproduza wengi ambao kwa sasa wanafanya kazi ukijaribu kuwauliza wengi wanafanya bure,” ameiambia Daladala beat ya Magic FM na kuongeza.

“Kwa hiyo sijaona umuhimu wa kufanya kazi bure, sasa hivi nipo serious kibiashara ndio maana unaona kama speed imepungua kutokana tabia za wasanii wetu hapa Bongo zipo hivyo,” amesisitiza Aby Dad.

By Peter Akaro

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents