Michezo

Sijawahi kumwambia mtu nataka milioni 150 – Obrey Chirwa

Mshambuliaji wa klabu ya Yanga raia wa Zambia, Obrey Chirwa amekana kuhitaji kiasi cha shilingi milioni 150 katika mkataba wake mpya nakusema kuwa watu ndiyo wanamzushia maswala hayo.

Mshambuliaji wa klabu ya Yanga SC, Obrey Chirwa akifanya mazoezi mepesi

 

Mshambuliaji huyo wazamani wa klabu ya FC Platinum amefika mbali zaidi na kusema kuwa kuumia kwake katika mchezo dhidi ya Majimaji kunahusishwa na kugoma kwake nbdani ya kikosi cha Yanga SC.

“Sijawahi kusema wala kumwambia mtu yeyote kuwa nataka 150M kwa ajili ya mkataba mpya, sipendezwi na namna wanavyonizushia,nadhani nia yao ni kunigombanisha na wapenzi wa Yanga.

Niliumia kwenye mchezo dhidi ya Majimaji ajabu wanasema nimegoma, huu ni upuuzi,mimi ni mchezaji wa Yanga, mimi na klabu ndiyo wenye kujua hatima yangu ya baadae,niacheni nicheze mpira”. – OBREY CHIRWA.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents