Tia Kitu. Pata Vituuz!

“Sijawahi kuona simu kama hii Tanzania na duniani kote”

Kwa sasa hivi ukitaja simu nzuri na kisasa zaidi duniani huwezi kusita kuitaja Infinix S5 ambayo imeingia sokoni wiki mbili zilizopita.

Infinix S5 inakuwa ni toleo la kwanza la S-series lenye kamera 4 kwa nyuma zenye ukubwa wa Megapixel 16,5,2+AI Camera,  Huku kila kamera ikifanya kazi yake ili kuweza kukupatia picha nzuri na zenye ubora.

Mfumo wa Teknolojia ya Artificial intelligence (AI camera), wengi wamekuwa wakihoji kuhusiana na ufanyaji kazi wa teknolojia hiyo, Teknolojia ya AI inaiwezesha simu yako S5 kupiga picha zenye muonekano halisi ya mazingira husika mfano kama ni jangwani au baharini aunt hata Ua basi utapata picha zenye rangi halisi ya vitu hivyo.

Ukiachilia mbali ukubwa wa kamera zake na moja mbele yenye Megapixel 32, S5 imekuja na ukubwa wa ndani wa  hadi GB 64.

Kuhusu Betri, Ukiwa na simu hii unaweza kukaa mpaka siku tatu bila kuchaji huku ukiwa umewasha data, Kwani simu hii imekuja na betri lenye ukubwa wa 4000 mAp.

Baadhi ya wakazi wa jiji la Dar Es Salaam, Wakiongea kuhusu ujio wa simu hiyo wameeleza vitu tofauti tofauti vilivyowavutia kwenye Infinix S5.

“Sina muda mrefu tangu nianze kutumia simu za Infinix,  Lakini hii S5 jamaa wametisha sana hususani kwenye mambo ya picha yaani wameboresha sana, Sijawahi kuona simu kama hii Duniani,” amesema Juma Nassor mkazi wa Tabata, Dar es Salaam.

“Sijawahi kutumia Infinix katika maisha yangu, Ila hii S5 ina sifa nyingi zinazonishawishi kununua inatunza Sana chaji. Mara ya kwanza niliiona kwa mke wangu, Nikaanza kuitumia baada ya kupoteza simu yangu ya awali. Kuanzia hapo simu hii ilinishawishi sana kununua,  Infinix nawaelewa sana najipanga na Mimi ninunue ya kwangu”  Amesema  Godfrey Ngimbo.

“Hii simu nimeipenda zaidi kwenye Kamera na ukubwa wa ndani, Sijawahi kuona simu kama hii hapa Tanzania na duniani kote ambako nimetembea. Yaani hakuna kitu kilikuwa kinanikera kama napiga picha halafu naambiwa simu imejaa nifute vitu kwanza ndio nipige picha.” amesema Jacqueline Kessy.

“Yaani ninachowapendea Infinix wanatoa simu nzuri halafu bei iko poa. Yaani kwa sifa za S5 nilijua watauza bei kubwa, kumbe ni rahisi tu. Mwezi huu nachukua ya kwangu niende nayo Upareni siunajua ni msimu wa sikukuu huu,” amesema Peter Mdee.

Simu za Infinix zipo kwenye maduka yote ya simu Tanzania na zinapatikana kwa bei ya kuanzia laki 4.

Pitia HAPA kusoma sifa za Infinix S5.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW