Burudani

Sijawahi kutamani kufanya kolabo na Alikiba – Harmonize

Msanii kutoka label ya WCB, Harmonize amefunguka iwapo yupo tayari kufanya kolabo na Alikiba.

Muimbaji huyo amesema hajawahi kutamani kufanya kolabo na msanii huyo na si Alikiba pekee bali na wasanii wengi.

“Lengo la Watanzania wote ni kuona ni kiasi gani tunaweza ku-push muziki wetu na kuupeleka mbali. Sijawahi kutamani kufanya kolabo na Alikiba, sijawahi kutamani kufanya kolabo na msanii yeyote lakini ikitokea kipindi tunafanya,” amesema.

“Vitu vingine lazima viwepo ili game izidi kupamba moto, so mimi sidhani kama kuna kitu cha ajabu sana,” Harmonize ameiambia Radio Five.

Kwa sasa Harmonize anafanya vizuri na kolabo aliyofanya na Diamond inayokwenda kwa jina la Kwa Ngwaru, huu ni wimbo wa pili kufanya pamoja baada ya ule wa Bado uliotoka mwaka 2016.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents