Moto Hauzimwi
Shinda na SIM Account

Sijawahi kuwa na matatizo na Alikiba, ni midomo ya watu tu – Barakah The Prince

Msanii wa muziki Bongo, Barakah The Prince amesema hajawahi kuwa na tofauti yoyote na Alikiba bali watu tu ndio huwa wanaeneza maneno.

Muimbaji huyo aliyejitoa katika label ya RockStar4000 ambayo Alikiba ni miongoni mwa wasimamizi, amelazimika kufunguka hayo baada ya kumtakia kheri ya siku ya kuzaliwa Alikiba wakati kukiwa na tetesi kuwa hawaelewani.

Barakah ambaye anatamba na ngoma ‘Sometimes’ ameiambia E-Newz, EATV kuwa hilo kila mtu anaweza kulichukuliwa kwa matazamo wake ila yeye hana tofauti na Alikiba kisa kuondoka RockStar4000.

“Sijawahi kuwa na matatizo na Alikiba na sijawahi kufikiria kuwa na matatizo naye, hayo amatatizo ni midomo tu ya watu wanatengeneza. Kuondoka kwenye kampuni yao ya kazi siyo kwamba na matatizo nao, hii ni kazi tu naweza nikahama ofisi yoyote” amesema Barakah.

Ameongeza kuwa kila mtu anaweza kuichukulia tofauti lakini yeye huwa anaishi bila kuangalia amemridhisha nani au kufanya kwa ajili ya nani kwa sababu anajua hayo ndio maisha yake na wapi anataka kufika.

Leave a comment

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW