Burudani

Sijui kama kuna Hip Hop ngumu na laini – Joh Makini (+video)

Rapper Joh Makini kutoka kundi la Weusi amesema kuwa hafahamu iwapo kuna hip hop ngumu au laini.

Kauli ya rapper huyo inakuja baada kuibuka maneno kuwa kundi la Weusi limebadili muziki wao hasa pale alipotoa wimbo wapo mpya uitwao Mdundiko.

“Ukiniambia kuna hip hop ngumu, kuna hip hop laini i don’t know which talk about,” amesema.

“Sisi tunachokifanya siku zote ni kile kile ila tunakifanya tofauti na kuendelea kukiboresha zaidi,” Joh Makini ameiambia Bongo5.

Wimbo wa Mdundiko umefanikiwa kuwakutanisha wasanii wanne kutoka Weusi tofauti na ilivyozoeleka kazi nyingi kufanya Joh Makini, Nikki wa Pili na G Nako. Safari hii Bonta kahusika pia.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents