Michezo

Siku za Omog za hesabika Simba SC

Mabingwa wa Kombe la Azam Sport Federation Cup ‘ASFC’, Simba SC inatarajia kucheza mchezo wake wa duru la tatu wa Ligi Kuu Tanzania Bara namba 24 dhidi ya klabu ya Mwadui FC utakao pigwa katika dimba la Uhuru Jijini Dar es salaam.

Simba itaingia uwanjani huku ikiwa na kumbukumbu ya kutoka sare tasa ya bila kufungana katika mchezo uliyopita dhidi ya matajiri wa Dar es salaam klabu ya Azam FC mchezo namba 10 wa duru la pili uliyopigwa Azam Complex Chamazi Agosti 9 mwaka huu.

Kufuatia matokeo ya kutoridhisha ya Simba tangu ilipoanza kuwatambulisha wachezaji wake katika mchezo wao wa Simba Day, mashabiki wa klabu hiyo wamekuwa wakilalamika katika mitandao ya kijamii kwa Kocha Mkuu, Joseph Omog kushindwa kupanga kikosi chake kilicho jaa wachezaji wenye majina makubwa hii inatokana na usajili bora uliyofanywa na timu hiyo msimu huu uliyogharimu zaidi ya Bilioni moja.

Katika mchezo wake wa Simba Day kikosi hicho kilichosheheni wachezaji wenye uzoefu mkubwa kilishindwa kufanya vizuri na kulazimika kuibuka na ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya timu ya Rayon Sports ya Rwanda bao lililofungwa na Mohamed Ibrahim dakika ya 16 kipindi cha kwanza.

Baada ya utambulisho wa wachezaji wake 10 wapya wakiwemo, Haruna Niyonzima na Emmanuel Okwi ikaingia uwanjani Agosti 23 katika mchezo wa Ngao ya Jamii ambao hutumika kufungua pazia la Ligi Kuu walipo cheza dhidi ya mahasimu wao Young Africans, klabu hiyo yenye maskani yake mtaa wa msimbazi ilishindwa kuonyesha makucha yake ya usajili mbele ya mashabiki lukuki waliyojaa uwanja wa Taifa walioamini kuchomoza na ushindi mnono hatimaye kumalizika kwa hatua ya matuta ya mabao 5-4 na kutwaa Ngao hiyo.

Mchezo uliyofuata Simba ikicheza na Mtibwa Sugar ikachomoza na ushindi wa bao 1-0 matokeo ambayo hayakutarajiwa na mashabiki wengi ukilinganisha hasa na uwekezaji uliyofanywa na timu hiyo msimu huu wa 2017/18.

Mara baada ya kuanza kwa msimu wa Ligi Kuu Tanzania Bara Simba ikacheza mchezo wake wa kwanza dhidi ya Ruvu Shooting na kufanikiwa kuchomoza na ushindi mnono wa mabao 7-0 na kuwafurahisha mashabiki wake ambao waliyoonekana kukerwa na matokeo yaliyopita.

Katika mzunguko wa pili wa Ligi kuelekea mchezo wao na Azam FC, klabu ya Simba ilipata fursa ya kucheza michezo kadhaa ya kirafiki ambapo ikicheza na baadhi ya timu kutoka Zanzibar, ikicheza na Gulioni FC na Mlandege zote za Visiwani. Kisha kucheza na Azam na kupata matokeo ya sare matokeo ambayo yameonekana kuzua maswali mengi ya wapenzi wa timu hiyo na kuamini kuwa Kocho Mkuu, Joseph Omog ameshindwa kupanga kikosi hasa msimu huu ukilinganisha na uwezo mkubwa wa wachezaji waliyopo.

Simba SC inaelekea katika mchezo wake na Mwadui siku ya Jumapili huku kuna umuhimu mkubwa kwa timu hiyo kuondoka na pointi tatu ili kutuliza presha ya mashabiki wanao amini ubora wa kikosi chao licha ya kwamba watawakosa wachezaji  wao wanne walio majeruhi, Haruna Niyonzima, Juma Liuzio, Erasto Nyoni na Shomari Kapombe.

Wakati mashabiki wakiendelea na wimbo wa kusisitiza kwa benchi la ufundi kumchezesha kiungo, Jonas Mkude nafasi ya kucheza mara kwa mara  msimu huu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents