Burudani

Sikufikiria kwamba Alikiba atakuwa amenisahau – Abdu Kiba

Msanii wa muziki Bongo, Abdu Kiba amefunguka sababu za ukimya wake kabla ya kutoa ngoma ‘Single’.

Alikiba na Abdu Kiba

Muimbaji huyo ameiambia E-Newz, EATV kuwa menejimenti (King’s Music) ndio ilipendekeza awe kimya ili atakaporudia awe na kitu kipya na siyo kwamba Alikiba alikuwa amemsahau kama inavyokuwa ikizungumzwa.

“Kwa upande wangu sikufikiria kwamba Brother atakuwa amenisahau ila mimi nilikubaliana na matakwa ya menejiment, kwamba natakiwa kukaa kimya kwa kipindi, hata mwaka ili nikirudi watu waone amerudi Abdu mpya” amesema.

“So nilipokubali hayo matakwa kilichotokea wakaweza kuzungumza kama walivyozungumza lakini mimi siyajali ni maneno tu ambayo waswahili wanasema hata kwenye kanga yapo” amesisitiza Abdu Kiba.

Abdu Kiba kwa sasa anatamba na ngoma ‘Single’ ambayo amemshirikisha Alikiba.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents