Habari

Sikukuu ya Krismasi yamuendea kombo Mhe. Nape Nnauye

Leo Desemba 25, 2017 ni siku ya furaha kwa wakristo wote duniani ambapo wanaadhimisha siku ya kuzaliwa bwana Yesu Kristu kama inavyotambulika kwa jina la Sikukuu ya Krismasi.

Mbunge wa jimbo la Mtama, Mh Nape Nnauye.

Wakati furaha hiyo ikiwa kwa watu wengi lakini sio siku nzuri kwa Mbunge wa Jimbo la Mtama, Mhe. Nape Nnauye ambaye amefiwa na rafiki yake pia Kada wa CCM namba moja jimboni kwake ambaye alimsaidia kwa kiasi kikubwa katika kampeni zake za kuusaka Ubunge kwenye uchaguzi mkubwa wa mwaka 2015.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa Twitter amethibisha hilo kwa kuandika “Nakulilia kaka yangu Mayage! Nilizunguka nawewe ziarani nikiwa Mwenezi, nilijifunza mengi sana kwako! Pumzika kwa amani kada wa kweli wa CCM na mkweli sana, hata pale ukweli unapouma! Binafsi natambua mchango wako! RIP!“.

Mungu akupe nguvu Mhe. Nnauye katika kipindi hiki kigumu kwa kuondokewa na moja ya makada wakubwa wa Chama chako.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents