Burudani

Sikupata bahati nyimbo zangu kupigwa kwenye radio – Mbosso

Msanii wa Bongo Flava, Mbosso amesema yeye ni miongoni mwa wasanii ambao hawakubata bahati kwa nyimbo zao kusikika katika radio station kwa kiasi kikubwa.

Muimbaji huyo ameendelea kwa kusema hata hivyo bado muziki wake umeweza kusikika kitu ambacho anashukuru.

“Ukizungumzia moja ya wasanii ambao hawakupata bahati ya kupata nafasi kubwa kwenye radio station, mimi pia naweza kusema nipo,” amesema.

“Sikupata bahati kabisa nyimbo kupigwa kwenye radio station lakini wananchi wamenipokea, wamesema Mbosso tunakusapoti, wamenisapoti nashuru leo nimefika nilipofika,” Mbosso ameiambia Bongo5.

Utakumbuka Mbosso mwaka ndipo amejiunga na label ya WCB inayomilikiwa na Diamond Platnumz. Kuna media nne ambazo hazichezi kazi za wasanii wote waliochini ya label hiyo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents