Michezo

Sikutamani kukutana na Chelsea – Valverde

Kocha mkuu wa Barcelona, Ernesto Valverde amesema kuwa alitamani timu ya Chelsea ingeshinda katika kundi lake na kuongoza ili tu asikutane nayo katika hatua hii ya 16 bora kwakuwa kila wanapokutana wanakuwa na wakati mgumu kwao dhidi ya mabingwa hao watetezi wa Uingereza.

Akizungumza na vyombo vya habari, Valverde amesema alitarajia kuikwepa Chelsea katika hatua hizi za awali lakini amesisitiza kuwa wachezaji wake wapo tayari kwajili ya mchezo huo.

“Tulitarajia Chelsea wangeshinda na kuongoza kundi na wangefanikiwa hilo tusingekutana nao, lakini tunakuwa na wakati mgumu sana tunapokutana nao,” amesema Valverde.

‘”Wamekuwa katika kiwango kizuri Hazard, Morata, Pedro na Willian wana ubora wa hali ya juu hapa nawazungumzia mabingwa wa sasa wa ligi ya Uingereza ambao tunakwenda kukutana nao.”

Timu hizi zilitoka sare michezo yake ya mwisho na kumaliza nafasi ya pili wakati Chelsea wakiwa nyuma ya Roma katika kundi C  na sasa wachezaji wa Barcelona wapo katika dimba la Stamford Bridge wakijiandaa dhidi ya wenyeji wao mchezo unaotarajiwa kupigwa leo siku ya Jumamosi usiku.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents