Burudani

‘Sikuwahi kuwa na mahusiano na Malaika’ – Timbulo

Msanii Timbulo hit maker wa ngoma ya ‘Mfuasi’, amefunguka na kusema hakuwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na msanii Malaika, na si kweli ugomvi wa kimahusiano ndio ulipelekea Malaika kutoonekana kwenye video ya wimbo wake ‘Ngomani’.

Timbulo na Malaika

Timbulo amekiambia kipindi cha The Play List cha Times Fm kuwa alifahamiana na Malaika kabla ya msanii huyo kutoka kimuziki na walikuwa wakisaidia mambo mbali mbali lakini ilifika kipindi wakapishana kwa sababu za kikazi na si vinginevyo.

“Malaika alifanya audio ya ngoma yangu alafu baadae kwenye video hakutokea, mimi nilivyokuja kuulizwa ikabidi nisema, ndio akaja kusema Timbulo anatafuta kiki na vitu vingine kibao. Hapana, kama ingekuwa ni mahusiano pengine hata ngoma isingefanyika the thing is panapotokea kitu lazima yatatokea mengi sana.

“Malaika ni miongoni mwa wasanii ambao nimekuwa naheshimiana nao na amekuwa kama mdogo wangu, nimefahamiana nae kabla hajawa msani mkubwa nilikuwa na sapoti yangu kidogo kwenye kile ambacho alikuwa anakifanya lakini baadae alikuja akasema sijawahi kumsaidia kitu,” amesema Timbulo.

By Peter Akaro

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents