Michezo

Si kweli kwamba ninashikiliwa na TAKUKURU – Hans Poppe

Mara baada ya hapo jana kufikishwa mahakamani rais wa klabu ya Simba Evans Aveva pamoja na makamu wake, Geofrey Nyange ‘Kaburu’  kufuatia tuhuma mbali mbali zinazo wakabili, jana kulikuwa na taarifa kwamba mwenyekiti wa kamati ya usajili ya klabu hiyo, Zacharia Hans Poppe alikuwa anashikiliwa na Takukuru.

Mwenyekiti wa kamati ya usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe

Hata hivyo Hans Poppe amesema alihojiwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) lakini akaachiwa na si anashikiliwa kama ambavyo imekuwa ikielezwa.

“Nilikwenda, nikahojiwa na baadaye nimeondoka, niko mitaani. Si kweli kwamba ninashikiliwa.

“Kuhusiana na kuhojiwa tayari nilihojiwa kama mara mbili hivi kabla. Haya ni mambo yanatokea,” alisema Hans Poppe.

Jana kulikuwa na taarifa kwamba Hans Poppe naye alikuwa anashikiliwa na Takukuru baada ya Rais wa Simba, Evans Aveva na Makamu wake, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ kupandishwa kizimbani.

BY HAMZA FUMO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents