Michezo

Simba hawarembi; Kocha mpya kutangazwa Jumatano, wadai maaandalizi ya mechi dhidi ya watani wao Yanga yapo tayari

Katika kuonyesha kuwa hawana muda wa kupoteza kuelekea mchezo wao dhidi ya watani wajadi Yanga SC, miamba ya soka ya Tanzania Bara Simba SC imesema kuwa maandalizi ya kuelekea mechi hiyo itakayopigwa mwezi Januari yapo tayari huku wakisema Kocha Mkuu wa klabu hiyo atakayerithi mikoba ya Patrick Aussems na benchi zima la ufundi litatangazwa siku ya Jumatano ya wiki hii inayokuja.

Mkurugenzi Mtendaji wa Klabu ya Simba Senzo Mazingiza

Hayo yamesema na Mkurugenzi Mtendaji wa Klabu ya Simba Senzo Mazingiza huku Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa klabu ya Simba, Mohammed Dewji akisitiza hilo la kutangazwa kwa Kocha mpya wiki ijayo kupitia Mkutano Mkuu wa Klabu ya Simba ulofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano ya Kimataifa ya Mwalimu Julius Nyerere,

“Tuna mchezo muhimu na watani wa jadi mwezi Januari. Napenda kuwahakikishia kuwa maandalizi na mambo yote ya mchezo huo yapo tayari. Wachezaji watakuwa kambini na tangazo la nani atakuwa kocha mkuu mpya na benchi la ufundi litatoka rasmi Jumatano ijayo.”- Amesema CEO wa Simba SC, Senzo.

Senzo Mazingiza ameongeza “Tupo mahali pazuri ambapo mishahara na posho mbalimbali vinatolewa kwa wakati. Wachezaji wetu wanalipwa vizuri ikilinganishwa na klabu kama Azam na Yanga ambao ni wapinzani wetu wakubwa. Kiwango cha pesa kinachotumika katika usajili na masuala mengine ni kikubwa pia.”

Wakati Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa klabu ya Simba, Mohammed Dewji akisema “Wiki hii, tunaleta kocha mpya, kocha mwenye kiwango kinachostahili kufundisha mabingwa wa nchi hii. Sasa tunaleta kifaa. Mtatangaziwa rasmi, ni nani, na anatoka nchi gani.”

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents