Michezo

‘Simba iko Kamili’ Okwi

 

Mshambuliaji wa timu ya Simba Emmanueli Okwi amesisitiza kwamba kwenye kambi ya timu yao iliyokuwa mjini Zanzibar hakuna


presha yoyote na wanaichukulia mechi dhidi ya Yanga leo,Agosti 18, kuwa ya kawaida. Okwi ambaye ni raia wa Uganda alisema wanaendelea na mazoezi kwanguvu na kila mmoja ana morali kuhakikisha ushindi unapatikana katika mechi hiyo.

“Huku hakuna mchecheto wowote sisi tumetulia tuli na kila mmoja anapanga mikakati jinsi ya kuikabili mechi n hiyo haimaanishi kwamba tunaogopa” alisema mchezaji huyo wa zamani wa SC VILLA. “Lengo ni kuhakikisha tunashinda kwavile sisi ni mabingwa watetezi na tunataka kuanza ligi vizuri.Ninavyoona mimi mpaka sasa, mambo yanaenda vizuri na tutashinda.Tumejiandaa vizuri sana na kila mmoja akili yake iko kimchezo,”alisisitiza mchezaji huyo.

Okwi akiwa kama tegemeo kwenye kikosi cha Simba, anategemezi kubwa la mashabiki kumfunga kipa Mghana wa Yanga ‘Yaw Berko’ ambaye ana nafasi kubwa ya kusimama langoni katika mchezo huo utakaopigwa kwenye uwanja wa Taifa.Mechi hiyo inasubiriwa kwa hamu na mashabiki pmoj na wadau wa soka wa Dar es salaam kwani wanaamini ndio itaonyesha ubora wa timu hizo mbili ambazo zimesajili mastaa kutoka nchi mbali mbali Afrika.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents