Uncategorized

Simba kumkabili Mtanzania Thomas Ulimwengu klabu bingwa Afrika

Mabingwa wa ligi kuu soka Tanzania Bara Simba SC watalazimika kukabiliana na Mtanzania Thomas Ulimwengu kwenye michuano ya klabu bingwa barani Afrika baada ya timu ya nyota huyo kupangwa kundi moja na wawakilishi hao wa nchi.

Siku tatu zilizopita klabu ya Jeunesse Sportive de la Saoura kutoka nchini Algeria ilimsajili mshambuliaji wa Kimataifa wa Tanzania, Thomas Ulimwengu kwaajili ya kuimarisha kikosi chake kwenye safu hiyo.

Sasa Simba ambao wapo kundi D ikiwa na timu za Al Ahly SC ya Misri, AS Vita Club ya DR Congo na Jeunesse Sportive de la Saoura ya Algeria italazimika kujiandaa vyakutosha kutokana na group hilo kuwa na klabu zenye asili ya Waarabu ambazo zimekuwa marakadhaa zikizisumbua sana timu za Tanzania kutokana na historia zinapokutana.

Miamba hiyo ya soka nchini imetinga hatua ya makundi baada ya kuifunga klabu ya Nkana FC kutoka Zambia kwa jumla ya mabao 4 – 3 kwenye michezo yote iliyocheza nyumbani na ugenini.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents