Michezo

Simba kutinga hatua ya robo fainali klabu bingwa Afrika, hii inakuwa mara ya ngapi kwa timu kufika hatua hii ? (+ Video)

Klabu ya soka ya Simba kutoka Tanzania imetinga hatua ya robo fainali ya Michuano ya Kabu Bingwa Afrika baada ya kusubiri kwa miaka 25. Mara ya mwisho kwa Simba kufikia hatua kama hiyo ilikuwa mwaka 1994, ambapo walitolewa na klabu ya Nkana ya Zambia kwa jumla ya magoli 4-3 baada ya kucheza michezo miwili.

Hiyo ilikuwa ni mara ya pili kwa Simba kufika robo fainali, mara ya kwanza ilikuwa miaka 45 iliyopita mnamo 1974 ambapo walisonga mpaka kufikia hatua ya nusu fainali na kutolewa na Ghazl Al-Mahalla ya Misri kwa mikwaju ya penati 3-0.

Na kufanikiwa kufuzu siku ya juzi jumamosi inakuwa ni mara ya tatu kufuzu katika michuanio hii.

By Ally Juma.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents