Michezo

Simba Kutumia CCM Kirumba

Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Tanzania bara wameamua kuhamishia mechi zao za ligi kwenye uwanja wa CCM kirumba jijini Mwanza.

Hatua hiyo ya Simba imetokana na uwanja wa uhuru jijini Dar waliokua wakiutumia na timu nyingine kama uwanja wa nyumbani kufungwa kwa ajili ya matengenezo.

Habari zilizopatikana klabuni hapo zinasema uongozi wa Simba ulichukua uwamuzi huo wa kwenda mwanza kutokana na masharti waliopewa na wamiliki wa wizara ya habari na utmaduni na michezo kuwa uwanja wa taifa unatakiwa utumike mara mmoja kwa wiki.

Chanzo hicho kilisema kutokana na sharti hilo la wamiliki wa uwanja wa Taifa (serikali) kamati ya utendaji ya Simba ilikutana juzi na kuamua kukubaliana kuhamia mwanza kwasababu ratiba iliyopo inaonyesha kwamba timu yao itakua na mechi mbili ndani ya wiki mmoja.

Alipoulizwa kuhusiana na taarifa hizo afisa wa Simba, Clifford Ndimbo alithibitisha na kusema kwamba ni kweli timu itahamia kwenye uwanja wa CCM kirumba jijini Mwanza.

 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents