Michezo

Simba kuwakabili mabingwa wa Morocco Ittihad Riadi De Tanger 

Simba kuwakabili mabingwa wa Morocco Ittihad Riadi De Tanger 

Wekundu wa Msimbazi Simba SC wakiwa nchini Uturuki wametangaza kucheza na Ittihad Riadi Tanger maarufu kama Ittihad Tanger ikiwa ni mchezo wake wa pili wa kirafiki wakiwa huko.

Simba itawakabili Ittihad Tanger ambao ni mabingwa wa sasa wa nchini Morocco hapo kesho siku ya Ijumaa ambao nao wapo Uturuki kwaajili ya maandalizi ya msimu wa ligi .

Mabingwa hao wa ligi kuu soka Tanzania Bara Simba wamethibitisha hilo kupitia ukurasa wao wa kijamii wa Instagram.

Kesho Saa kumi alasiri Mabingwa wa Nchi Simba Sports Club itacheza mechi ya pili ya kirafiki ikiwa nchini Uturuki.. Klabu ya Simba itacheza na Mabingwa wa sasa wa Morocco Ittihad Riadi De Tanger ambao nao wapo nchini Uturuki kwa maandalizi ya msimu ujao wa Ligi.

Katika mchezo wake wakwanza wa kirafiki dhidi ya Moulodia Oudja klabu ya Simba ilitoka sare ya goli 1 – 1 na mechi hiyo kuahirishwa kufuatia mvua kunyesha wakati mfungaji wa bao hilo akiwa Adam Salamba.

Related Articles

3 Comments

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents