Michezo

Simba kwa Yanga ‘Hii Kichapo Tu’

Kufuatia uchaguzi mkuu wa Yanga uliowaweka madarakani mwenyekiti Lioyd Nchunga na makamu wake Davis Mosha kuwa mahasimu wao wakubwa, Simba wamesema enzi zao za vipigo vitarejea jangwani. Habari zilizotolewa na baadhi ya wadau wa wekundu wa msimbazi kwa bongo5 wamesema awali,walijua wanachama wa yanga wangempa uongozi Kifukwe au Igangula watu pekee wenye uzoefu wa fitina za zoka lakini kwa hawa wasasa wasahau kuifunga simba.

 

“Zile enzi zetu zakushinda kwa miaka mingi mfululizo maana zimewadia. Madrga alijitahidi kidogo kuzuia,lakini kwa Nchuga na Mosha ingawa ni viongozi wazuri lakini wasahau kuifunga Simba ,alisema kiongozi mmoja”.

Kiongozi mwingine alisema aliposikia ushindi kwa wagombea hao waligonganisha glasi za kujipongeza mapema asubuhi ya Jumatatu.

“Usiku mzima tulikua tunafuatilia kujua nani atashinda.Habari za kujitoa kwa Kifukwe zilitufanya tuanze kunywa champagne na matokeo ya mwisho ndio kabisaa tukagonganisha glasi kwa furaha”.

 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents