Michezo

Simba na Yanga kukutana leo nusu fainali ya kombe la Mapinduzi

Nusu fainali ya kombe la Mapinduzi yanayo fanyika mjini Zanzibar, itafanyika leo kati ya mchezo wa wapinzani wa jadi Simba na Yanga unaotarajiwa kufanyika leo katika uwanja wa Aman majira saa mbili na robo usiku.

Mchezo huo unao subiriwa kwa hamu na wadau wengi wa soka utakuwa wa kwanza kwao kukutana kwa mwaka 2017 kwenye kombe la Mapinduzi.

Timu ya Yanga wanaingia kwenye mchezo huo wakiwa na majeruhi baada ya kupata kipigo cha magoli 4 kwa bila dhidi ya Azam, wakati Simba wao wakiwa na rekodi nzuri kwenye mashindano hayo wakiwa hawaja poteza mchezo hata mmoja.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents