Michezo

Simba ndio bingwa msimu huu – Haji Manara

Aliyekuwa msemaji wa klabu Simba SC Haji Manara, amendelea kujitapa kuwa klabu yake ndio bingwa wa ligi kuu soka Tanzania bara kwa msimu wa 2016/17 na kuwataka wapinzani wao wa jadi kujipanga.

Haji Manara

Kupitia mitandao ya kijamii Manara ameandika, ‘wabongo bana kwa ‘double standard’ hawajambo, Serengeti Boys walikuwa Gabon kwa kushinda rufaa ila Simba hawastahili. Mjiandae kiakili Gongowazi, Simba ndiyo ‘champion’ msimu huu”.

Simba kwa sasa inasubiri majibu ya rufaa waliyoikatia klabu ya Kagera Sugar katika Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) kwa kile walichodai klabu hiyo ilimchezesha mchezaji mwenye kadi tatu za njano, kitu ambacho ni kinyume cha sheria za mpira wa miguu. Hata hivyo wapinzani wao, Yanga siku ya Jumamosi walikabidhiwa kombe kama mabingwa wa msimu wa 2016/17.

By Peter Akaro

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents