Simba SC ipotayari kuwafuata Waarabu

Vinara wa ligi kuu soka Tanzania Bara Simba SC wanatarajia kuondoka hii leo majira ya saa 10:00 jioni kwenda nchini Misri kupitia Shirika la ndege la Ethiopian Airlines kuwakabili Al Masry michuano ya kombe la Shirikisho Barani Afrika.

Kikosi hicho kinachojiandaa na mchezo huo wa kimataifa kimefanya mazoezi yake ya mwisho asubuhi ya leo katika uwanja wa Boko jijiini Dar es Salaam kabla ya kuanza safari kuelekea nchini Misri.

Simba SC inakwenda kuwakabili Waarabu hao huku wakiwa na kumbukumbu ya kutoka sare ya mabao 2 – 2 kwenye mchezo wa awali uliyopigwa hapa nyumbani katika dimba la Taifa jijini Dar es Salaam wakati washambuliaji wake mahiri, John Bocco na Emmanuel Okwi wakichomoka na bao moja kila mmoja wakati wekundu hao sasa watalazimika kuchomoza na ushindi wa 2 – 0 ili kujihakikishia nafasi ya kusonga mbele.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW