Michezo

Simba SC kibaruani leo ligi kuu

Klabu ya soka ya Simba SC, hii leo itajitupa uwanjani kuwavaa chama cha wana klabu ya Stand United katika michuano ya Ligi kuu soka Tanzania Bara, katika mchezo utakaopigwa katika Dimba la Uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam jioni ya leo.


Wachezaji wa klabu ya Simba Sc

Mchezo wa leo utatoa tafsiri kubwa katika msimamo wa ligi kuu VPL. Endapo klabu ya Simba itachomoza na ushindi katika mchezo huo, itarudi tena kileleni na kuendelea na matumaini yao ya kunyakua kombe la ligi kuu.

Endapo Simba SC itapoteza mchezo, itatoa tafsri ya wazi kuwa sasa bingwa wa ligi kuu Bara itakuwa klabu ya Yanga, kwani itakuwa imesalia na michezo mingi zaidi ya klabu ya Simba huku ikiwa inaongoza kwa tofauti ya magoli ya kufungwa na kufunga.

Hivyo tunaweza kusema leo ndio leo katika ligi kuu, matokeo yoyote yatakayojiri katika mchezo itatoa hali ya ligi hii inapoelekea huku tukielekea ukomo wake hivi karibuni. Wekundu hao wa Msimbazi watacheza mechi yao ya 29 leo watakapowakaribisha Stand United, huku wakihitaji kushinda ili kuweka hai matumaini ya ubingwa.


Mashabiki wa klabu ya Simba Sc wakishabikia Timu yao

Kikosi hiko cha kocha raia wa Mcameroon, Joseph Marius Omog ina alama 62, sawa na mabingwa watetezi, Yanga Sc wenye alama 62 ambao wapo kileleni kwa wastani wao mzuri wa mabao na pia wana mechi moja mkononi.

Katika upande wa pili matajiri wa Daresalaama, wakoka mikate, klabu ya Azam FC watakuwa wenyeji wa klabu ya Toto Africans, mchezo utakaopigwa kando kando ya mji huko Azam Complex, Chamazi.

Na hapo kesho klabu ya Yanga itakuwa kibaruani kumenyana na timu ya jiji, klabu ya Mbeya City huku Mtibwa Sugar wakiwa wenyeji wa Mwadui FC Uwanja wa Manungu, Turiani, Morogoro.

Mechi nyingine za kesho ni kati ya Tanzania Prisons na Ndanda Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya na Jumapili African Lyon itamenyana na Ruvu Shooting. JKT Ruvu na Maji Maji ya Songea Uwanja wa Maji Maji,

BY HAMZA FUMO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents