Michezo

Simba SC kuanza kutoa elimu kwa mashabiki wake leo

Jumatano hii uongozi wa klabu ya soka ya Simba SC umepanga kuanza kutoa semina kwa mashabiki wake kuhusu kujenga uelewa mpana zaidi juu ya muundo mpya wa klabu hiyo.

Mkuu wa kitengo cha Habari na Mawasiliano wa timu hiy Haji Manara ametoa taarifa hiyo kuwa semina hiyo itafanyika katika ukumbi wa Mikumi uliopo katika viwanja vya Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara ya Sabasaba (PTA), Kurasini jijini Dar es Salaam.

TAARIFA KWA UMMA

Klabu ya Simba kesho inatarajiwa kufanya Semina kubwa ya Wanachama wote wa klabu hiyo.
Semina hiyo inalenga kujenga uelewa mpana zaid juu ya muundo mpya wa klabu, uliotokana na mabadiliko ya katiba yaliyofanywa na wanachama hao,na kusajiliwa na Msajili wa Vilabu nchini.
Maandalizi yote ya Semina hiyo yamekamilika,na itafanyika kesho tarehe 16-8-2017,Jumatano Saa Nane na Nusu mchana(8.30) na itafanyikia kwenye ukumbi wa Mikumi uliopo kwenye eneo la maonyesho ya kimataifa ya biashara ya Sabasaba (PTA) kurasini hapa jijini Dar es salaam.
Tunawaomba wanachama wote popote walipo waje kwa wingi hapo kesho, huku klabu ikiwaomba viongozi wa Simba Wilaya ya Temeke waandae utaratibu mzuri wa kuwapokea wageni.
IMETOLEWA NA…. HAJI S MANARA

MKUU WA HABARI SIMBA SC
SIMBA NGUVU MOJA

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents