Michezo

Simba SC kukipiga na wababe wa Dodoma Jumatano hii

Baada ya kuifunga Stand United ‘Chama la Wana’ na kushika usukani wa msimamo wa Ligi Kuu Vodacom Tanzania Bara, Simba SC hapo kesho siku ya Jumatano Oktoba 4, watashuka dimbani kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Dodoma FC Uwanja wa Jamhuri Dodoma.

Kocha mkuu wa timu hiyo ya wekundu wa Msimbazi, Joseph Omog atatumia nafasi hiyo muhimu kukitathimini kikosi chake katika kipindi hiki ambacho VPL imesimama kupisha mchezo wa kalenda ya FIFA.

Omog atavaana na kocha mwenye historia na Simba na  mwenyemaneno mengi katika mchezo wa soka hapa nchini Jamhuri Kiwhelo Julio ‘Pereira’ ambaye amakinoa kikosi cha Dodoma FC ambacho kinashiriki Ligi daraja la kwanza Tanzania Bara ‘FDL’.

Katika mchezo uliyopita wa Ligi Kuu Tanzania Bara timu ya Simba SC iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 huku mchezaji, Shiza Ramadhan Kichuya na Laudit Mavugo wakipachika magoli hayo na kuifanya kukwea kileleni kwa pointi 11.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents