Michezo

Simba SC watua Kenya kushiriki michuano SportPesa Super Cup 2018

Mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2017/18, Simba SC mchana wa leo (Mei 31 2018) wametua nchini Kenya kwaajili ya kushiriki michuano ya SportPesa Super Cup 2018.

Michuano hiyo ambayo inashirikisha timu 8, nne kutoka Tanzania ambazo ni Singida United, Simba SC, Yanga SC pamoja na JKU na nne kutoka Kenya ambazo ni AFC Leopards, Kariobangi Sharks, Gor Mahia pamoja na Home Boys.

Ratiba ya michuano hiyo inayotarajiwa kuanza kuunguruma Juni 3 mpaka 10, mwaka huu katika Uwanja wa Afraha mjini Nakuru, Kenya, tayari imetoka ambapo Yanga itafungua mashindano hayo kwa kumenyana na Kakamega Homeboys ya Kenya.

Mchezo huo umepangwa kuanza saa 7:00 mchana, huku Gor Mahia ambayo nayo ni ya Kenya ikipambana na JKU ya Zanzibar kuanzia saa 9:15 alasiri. Mechi hizo zote zitachezwa Juni 3.

Simba ya Tanzania, wao watacheza siku inayofuata dhidi ya Kariobangi Sharks ya Kenya mchezo utakaopigwa majira ya saa 9:00 alasiri ambapo siku hiyo itachezwa mechi hiyo pekee. Juni 5, AFC Leopards ya Kenya itakutana na Singida United kutoka Tanzania.
Mmoja wa waratibu wa michuano hiyo, Sabrina Msuya, alisema, maandalizi yote yako vizuri na timu kutoka Tanzania ambazo ni Simba, Yanga na JKU zinatarajiwa kuondoka kesho Alhamisi, huku Singida United ikisubiri mpaka imalize mechi yake ya Kombe la FA itakayochezwa Jumamosi hii.

“Mambo tayari yako safi kabisa kwani ratiba imetoka na timu za hapa nchini zitaondoka Alhamisi kuanzia saa 3:00 asubuhi ambapo Simba ndiyo itakuwa ya kwanza ikifuatiwa na JKU ambayo itaondoka Saa 7:00 mchana na baadaye saa 11:00 jioni, Yanga itafuatia.

“Singida United yenyewe itaondoka mara tu baada ya mchezo wake wa FA unaotarajiwa kufanyika Juni 2, mwaka huu huko Arusha,” alisema Sabrina.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents