Michezo

Simba SC yachukua ubingwa wa Ngao ya Jamii mbele ya Yanga

Klabu ya Simba SC imechukua ubingwa wa Ngao ya Jamii 2017 kwa mikwaju ya penati dhidi ya watani wao wa jadi Yanga SC katika mchezo uliochezeka Jumatato hii ndani ya dimba la uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Mashabiki wa Simba wakishangilia ubingwa.

Wekundu hao wa Msimbazi wamechukua ubingwa huo baada ya kushinda penati 5 kwa 4 kati ya penati 6 zilizopigwa

Mchezo huo ulianza kwa vuta nikuvute mpaka dakika 45 za kipindi cha kwanza mpira ulimalizika bila timu hizo kufungana huku beki wa wekundu hao, Method Mwamjale akipewa kadi ya njano katika dk 35 ya mchezo baada ya kuonyesha nidhamu mbaya kwa mwamuzi wa mchezo huo, Elly Sasii.

Katika kipindi cha pili mchezo ulianza kwa kasi kila mmoja akitaka kuona nyavu za mwenzake bila mafanikio huku kila mmoja akionekana kumkamia mwenzake hali iliyopelekea mchezo huo kamalizika bila kufungana na kuingia kwenye mikwaju ya penati.

Makocha wazungumza.

Akiongea na waandishi wa habari muda mchache baada ya kumalizika kwa mchezo huo, Kocha wa Simba Joseph Omog amesema ushindi huo unaonyesha ni jinsi gani wamejipanga vizuri kwaajili ya mchezo wao ujao.

“Mchezo ulikuwa mzuri sana na mwisho wa siku tumechukua ubingwa wa Ngao ya Jamii hii ni dalili mzuri kwa timu yetu katika msimu wetu ujao. Kikubwa tayari tumewaona wachezaji wetu wapya, wamecheza vizuri licha ya baadhi ya wachezaji wetu wapya kama John Bocco amekosa mchezo wa leo,” alisema kocha wa Simba .

Viongozi wa Yanga na wachezaji wakichukua medali.

Kwa upande wa kocha msaidizi wa Yanga, Shadrack Nsajigwa amesema mchezo huo ulikuwa mzuri na wakuvutia ingawa wamepoeza kwa mikwaju ya penati.

Kocha huyo amesema kikosi chake kimecheza vizuri licha ya kuwa na wachezaji wapya wengi ambao sio wazoefu huku akidai watautumia mchezo huo kwa maandalizi ya msimu mpya wa ligi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents