Michezo

Simba SC yaendeleza ubabe VPL yaiadabisha Azam FC

Klabu ya Simba yaibuka na ushindi wa bao 1 – 0 dhidi ya Azam FC mchezo wa ligi kuu soka Tanzania Bara.

Bao la Simba SC likifungwa na mshambuliaji wa kimataifa wa Uganda, Emmanuel Okwi kunako dakika ya 37 kipindi cha kwanza.

Kwa matokeo hayo Simba SC inaongoza katika msimamo wa ligi  kwa kuwa na jumla ya pointi 41 na kuweka rekodi ya kutopoteza hata mchezo mmoja mpaka sasa nafasi ya pili ikishikiliwa na Yanga SC wenye alama 33.

Katika michezo mengine iliyopigwa hii leo Katika dimba la Majimaji mjini Songea, mchezo umemalizika kwa suluhu. Majimaji FC 0-0 Tanzania Prisons

Wakati katika dimba la CCM Kambarage mjini Shinyanga, Lipuli FC wanaibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Stand United.

Huko katika dimba la CCM Kirumba, Singida United wanaondoka na pointi zote tatu kwa ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mbao FC.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents