Michezo

Simba SC yafanya mazoezi ya mwisho kuikabili Prisons

By  | 

Mabingwa wa kombe la shirikisho (FA) klabu ya Simba leo imefanya mazoezi yake ya mwisho kabla ya kuikabili timu ya Tanzania Prison hapo kesho siku ya Jumamosi.

Simba SC ambayo inaongoza ligi kuu soka Tanzania Bara kwa kuwa na pointi 19 itashuka dimbani kesho katika mchezo wa mzunguko wa 10 kutafuta alama tatu muhimu dhidi ya wenyeji wao Tanzania Prison.

Kupitia mtandao wake wa kijamii Simba SC imesema kuwa leo imefanya mazoezi yake ya mwisho.

“Kikosi cha Simba leo Asubuh kimefanya mazoezi yake ya mwisho tayari kujiandaa na mchezo wa kesho dhidi ya Tanzania Prison.”

Simba SC ikiwa inaongoza msimamo wa ligi kwa kuwa na alama 19 ikifuatiwa na Azam FC wenye pointi 19 itawakabili wenyeji wao ambao wanashika nafasi ya sita kwa kuwa na alama 14.

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Add a comment

comments