Michezo

Simba SC yamalizana kibabe na Patrick Aussems ‘Uchebe’, apewa kandarasi mpya ya mwaka mmoja 

Kocha Mkuu wa klabu ya Simba, Patrick Aussems hapo jana ameingia kandarasi mpya na timu hiyo na kuendelea kuitumikia miamba hiyo ya soka kutoka mitaa ya Karia Koo.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo, Aussems ameingia mkataba wa mwaka mmoja baada ya kutimiza yale aliyotakiwa kuyatekeleza kutoka kwenye kandarasi iliyopita.

”Kocha Patrick Aussems amesaini mkataba mpya wa mwaka mmoja kuendelea kuwa Kocha Mkuu. Uamuzi wa kumuongezea mkataba umefikiwa na Bodi ya Wakurugenzi baada ya Kocha Aussems kufikia malengo aliyowekewa katika mkataba unaomalizika hivi karibuni ya kuhakikisha timu inatetea ubingwa wa Ligi Kuu na inafika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Pichani ni Kocha Aussems akisaini mkataba na pembeni ni Mwenyekiti wa klabu, Swedi Mkwabi na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Mohammed Dewji.#NguvuMoja  ” Taarifa kutoka ndani ya klabu ya Simba.

Katika taarifa hiyo iliyotolewa na uongozi wa Simba zinaonyesha Patrick Aussem akisajili mkataba huo na miamba hiyo ya soka ya Tanzania.

Kwenye mkataba wake uliyomalizika ulimtaka, Patrick Aussems alitakiwa kuifikisha timu ya Simba hatua ya makundi ya klabu bingwa Afrika huku kuhakikisha inatetea ubingwa wake wa ligi kuu soka Tanzania Bara.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents