Michezo

Simba SC , Yanga SC zapangua ratiba VPL

Shirikisho la mpira wa miguu nchini (TFF) limebadili tena ratiba ya ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara kwa timu za Simba SC na Yanga SC ambazo zipo katika michuano ya kimataifa.

Mchezo wa Simba SC dhidi ya Stand United umerudishwa nyuma hadi tarehe 2 ya mwezi ujao badala ya Februari 4 ilivyo pangwa hapo awali ambao utachezwa katika dimba la uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Kurudishwa nyuma kwa mchezo huo ni kufuatia klabu ya Simba kupata nafasi ya kujiandaa na mchezo wake wa michuano ya kombe la Shirikisho dhidi ya Al Masry ambao unatarajiwa kupigwa Februari 7.

Hasimu wake Yanga SC haitashuka katika dimba la Jamhuri Morogoro kuikabili Mtibwa Sugar Februari 3 kama ilivyopangwa hapo hawali na badala yake tarehe ya mchezo huo itatajwa hapo baadaye.

Msimamo wa ligi kuu soka Tanzania Bara unaonyesha Simba SC inaongoza kwa kuwa na pointi 45 nafasi ya pili ikishikiliwa na Yanga SC yenye alama 37 wakati ya tatu ikiwa ni Azam FC yenye jumla ya pointi 35.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents