Michezo

Simba SC yarejea Dar na dawa ya Singida United

Kikosi cha Simba leo asubuhi kimeanza safari ya kurejea jijini Dar es Salaam tayari kwa mchezo wake dhidi Singida United kikitokea Mkoani Morogoro ambako kiliweka kambi yake kwaajili ya maandalizi ya Vpl.

Kikosi cha Simba kikiwa chini ya kocha wake, Masoud Djuma kitashuka katika Uwanja wa Taifa huku kikiwa na nyotawake mshambuliajia raia wa Uganda, Emmanuel Okwi ambaye alikuwa akisumbuliwa na majeraha.

Simba SC inaongoza katika msimamo wa ligi kuu soka Tanzania Bara kwa kuwa na alama 26 sawa na wanalambalamba klabu ya Azam FC wakiwa na tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa.

Nafasi yatatu ikishikiliwa na Mtibwa Sugar wenye pointi 24 ya nne ikiwa chini ya Singida United na yatano wakishikilia mabingwa watetezi Young Africans wenye alama 21.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents