Michezo

Simba SC yarejea kileleni mwa ligi ya VPL

Ligi Kuu soka Tanzania Bara imeendelea hii leo kwa michezo kadhaa kupigwa katika viwanja mbalimbali huko Kaitaba Mkoani Kagera, klabu ya Simba imechomoza na ushindi wa mabao 2 – 0 dhidi ya Kagera Sugar.

Katika mchezo huo uliyokuwa na ushindani mkubwa hasa ukizingatia kikosi cha Kagera Sugar kina wachezaji wengi waliyopata kuichezea Simba kama vile Juma Nyoso,Juma Kaseja, Adeyum Salehe, Mohamed Fakhi na wenginewengi, mechi hiyo imemalizika kwa matokeo hayo ambayo unaifanya timu hiyo yenye maskani yake mitaa ya Kari Koo kurejea kileleni mwa ligi kwa kuwa na jumla ya pointi 32 ikiizidi Azam FC alama 2.

Waliyoikuwa mwiba mkali katika mechi hiyo na kuisaidia Simba SC kuchomoza na ushindi huo ni Said Ndemla na John Bocco waliyoibuka na bao moja moja kila mmoja.

Katika mchezo mwingine uliyopigwa hii leo ni kati ya timu ya Majimaji FC dhidi ya Singida United.

Katika mchezo huo Majimaji imetoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Singida United. 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents