Michezo

Simba SC yashushiwa rungu na kamati ya saa 72

Kamati ya Usimamizi na Uendeshaji wa Ligi (Kamati ya Saa 72) ya Bodi ya Ligi katika kikao chake kilichopita ilipitia taarifa na matukio mbalimbali na kufanya uamuzi ufuatao.

Klabu ya Simba imepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kutokana na kuonyesha vitendo vinavyoashiria ushirikina katika mechi hiyo iliyofanyika Aprili 3, 2018 kwenye Uwanja wa Sabasaba mjini Njombe, ikiwemo pia mshabiki mmoja wa timu hiyo kuingia uwanjani na kuchukua taulo la kipa wa Njombe Mji lililokuwa golini. Adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 42(1) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti wa Klabu.

Mechi namba 165 (Mtibwa Sugar 0 vs Simba 1). Klabu ya Simba imepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kutokana na washabiki wake kuingia uwanjani baada ya filimbi ya mwisho ya mechi hiyo iliyofanyika Aprili 9, 2018 kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.

Kitendo hicho cha washabiki wa Simba iliyokuwa ikicheza ugenini ni ukiukaji wa Kanuni ya 14(11) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo, wakati adhabu dhidi yao imezingatia Kanuni ya 14(49) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents