Michezo

Simba SC yatangaza kamati ya kusimamia mchakato wa zabuni

Kamati ya utendaji ya klabu ya Simba kupitia kwa Mkuu wake wa Idara ya Habari na Mawasiliano, Haji Manara imetangaza kamati maalumu ya kusimamia mchakato wa zabuni wa kumpata muwekezaji katika mfumo mpya wa umiliki timu hiyo.

Manara amesema hayo baada ya kupita siku chache toka mkutano mkuu wa Simba SC kupitisha maamuzi ya kubadilisha umiliki wake kutoka klabu ya michezo inayomilikiwa na wanachama na kuwa kampuni inayomilikiwa na wanahisa.

“Kamati ya utendaji ilikutana hivi karibuni na kuamua kuunda kamati ya kupitia mchakato wa zabuni wa kumpata mwekezaji au wawekezaji ambao ni wanachama wa Simba, watakaonunua hadi asilimia 50 ya hisa za klabu ya Simba”,amesema Manara.

 Haji Manara ameongeza “Katika zile asilimia 100, asilimia 50 zinapaswa ziuzwe kwa mwanachama wa Simba kwa mfumo wa tenda ambao kamati itakayosimamia shughuli hiyo imeshaundwa na leo ninaitangaza kamati hiyo ambayo itakuwa huru na haitaingiliwa katika mchakato huu”.

 “Uuzwaji huo utafanyika kwa kuzingatia sheria za nchi, tuna imani kubwa na timu hii tuliyoiunda kwa sababu ina watu wabobezi,” .

Soma zaidi

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents