AFCON 2019 Tupogo!
Vodacom Data Datani!

Simba SC yatangaza kufanya kisomo juu ya mlezi na mwekezaji wa timu hiyo, Mo Dewji 

Uongozi wa klabu ya Simba umetangaza kufanya kisomo hii leo siku ya Ijumaa huku lengo kuu ikiwa ni kumuombea Mwenyezimungu aweze kuleta wepesi kwenye matatizo yaliyompata mlezi na mwekezaji wa timu hiyo, Mohamed Dewji anaedaiwa kutekwa.

Uongozi wa Klabu ya Simba unapenda kuwataarifu Wanachama, Wapenzi na Washabiki wake kuwa mchana wa leo baada ya Sala ya Ijumaa (Saa 8.00) kutakuwa na *KISOMO* katika Makao Makuu ya Klabu Mtaa wa Msimbazi.

Lengo la *KISOMO* hiki ni kumuomba Mwenyezimungu aweze kuleta wepesi kwenye Matatizo yaliyompata Mlezi na Mwekezaji wetu Bw. Mohamed Dewji “MO”

Tunapenda kuwakaribisha katika Kisomo hiki muhimu ili kumuomba Mungu aweze kumlinda na kumrejesha Mwenzetu salama.

*Tunatanguliza Shukrani*

Kwa mujibu wa jeshi la polosi Mo ametekwa jana majira ya asubuhi alipokuwa akielekea kwenye mazoezi.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW