Michezo

Simba: Tutaongea Dakika ya 90

Uongozi wa Simba umesema kuwa wenzao Yanga wamekua na maneno mengi lakini wao watazungumza mara tu baada ya mechi kumalizika.

Akizungumza jana mwenyekiti wa klabu hiyo Ismail Aden Rage, alisema kuwa viongozi wa Yanga wamekuwa wakizungumza mengi kwenye vyombo vya habari lakini wao wako kimya,isipokuwa watakua tayari kuzungumza baada ya dakika ya 90.

Sisi tutasema baada ya dakika 90 kumalizika, wenzetu Yanga wamekuwa wakizungumza mengi kwenye vyombo vya habari lakini sisi tuko kimya. Baada ya mechi tutakua nay a kusema.

Alisema yeye na makamu wake Godfrey Nyange wamefanya maandalizi ya kina kwa ajili ya mechi hiyo ndio maana hawapigi kelele.

Alisema wachezaji wameandaliwa kisaikolojia kwa ajili ya mechi hiyo yote ili kuhakikisha timu yao Simba inapata ushindi.

 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents