DStv Inogilee!

Simba waalikwa nchini Oman mwezi ujao

simba-sports-club

Klabu ya Simba imealikwa kwenda nchini Oman mwezi ujao kwenda kushiriki kwenye tukio maalum lililoandaliwa huko.

Wenyeji wamekubali kuanzisha ushirikiano na Simba ambapo timu hizo zitakuwa zikitembeleana na ili kuongeza uhusiano kati ya Tanzania na Oman.

Simba itacheza na mabingwa wa ligi ya Omantel Elite timu ya Fanja katika shughuli ya siku moja ambapo baadaye Simba wataialika pia timu hiyo baadaye mwakani.

Mwenyekiti wa Simba Ismail Aden Rage alisaini makubaliano hayo mjini Muscat akiwa na mwenzake wa timu ya Fanja, Hamyar al Ismaily.

Katika safari hiyo Simba itakaa Muscat kwa muda wa wiki mbili.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW