Tupo Nawe

Simba waaza safari yao ya kuifuata TP Mazembe, Kochas Aussems atoa ya moyoni (+ Video)

Klabu ya Simba imesafiri leo asubuhi kuelekea Congo DR kwa ndege maalum ya kukodi kwa ajili ya mechi yao ya marudio ya CAF Champions League hatua ya robo fainali dhidi ya TP Mazembe ambayo inatarajiwa kuchezwa kesho Jumamosi.


Kwa mujibu wa meneja wa Simba Patrick Rweyemamu safari kutoka Dar hadi Lubumbashi itachua saa 3 hadi kuwasili.

https://www.instagram.com/p/BwJK1P1neHF/
“Tukifika tutajipanga kwa ajili ya kwenda kufanya mazoezi ya mwisho kwenye uwanja ambao tunategemea kuchezea mechi kujiandaa rasmi kwa ajili ya mchezo wa Jumamosi”-Patrick Rweyemamu.
“Mipango mingine yote inafanywa na uongozi na tayari kuna viongozi walishatangulia kwa ajili ya kuweka mambo sawa.”

Haya ni maneno ya Kocha kabla ya mchezo huo ambayo alitumia ukurasa wake wa Twitter kuyaandika:-

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW